Futa data yako
Kumbukumbu zako za SawaFone ziko kwenye simu yako tu. ETITE haina nakala kwenye seva yoyote, kwa hiyo hakuna cha kufuta upande wetu. Unafuta kila kitu wewe mwenyewe, ndani ya programu.
Ndani ya programu
- Fungua SawaFone na uguse Zaidi.
- Gusa Faragha na ruhusa.
- Gusa Futa data yangu.
- Soma kitakachofutwa, kisha uguse Futa kila kitu.
- Ikiwa simu yako ina kufuli ya skrini, ifungue ili kuthibitisha.
Haiwezi kutenduliwa. Ili kubaki na nakala, tumia kwanza Pakua data yangu, kwenye skrini hiyo hiyo.
Kinachofutwa
- kumbukumbu zako za pesa, vikumbusho, madokezo na orodha;
- watu wasio na simu;
- picha na faili za madokezo yako, na picha za risiti;
- mipangilio yako;
- kila nakala rudufu kwenye hifadhi ya SawaFone kwenye simu hii, na msimbo wako wa urejeshaji uliohifadhiwa.
Nakala ya nakala rudufu yako kwenye akaunti yako ya Google inaondoka simu yako itakapohifadhi nakala tena (kwa kawaida usiku, kwenye Wi-Fi, ikiwa inachajiwa).
Kinachobaki
- Anwani zako na matukio ya kalenda. Yako kwenye programu za Anwani na Kalenda za simu yako. Yafute huko ukitaka.
- Nakala uliyohifadhi mwenyewe, kutoka “Pakua data yangu” au nakala ya pili ya nakala rudufu (kwenye kadi ya SD au Google Drive). Ifute pale ulipoihifadhi.
Kuondoa programu
Kuondoa SawaFone pia kunafuta kila kitu inachohifadhi kwenye simu. Nakala ya nakala rudufu kwenye akaunti yako ya Google inafuata sheria za nakala rudufu za Google; imefungwa, na hakuna anayeweza kuifungua bila msimbo wako wa urejeshaji.
Unahitaji msaada?
Tuandikie kwa [email protected].
WhatsApp: +250 794 768 888.
Tunajibu ndani ya siku 30. Hatutakuomba kamwe msimbo wako wa urejeshaji.